Deuteronomy 34

Kifo Cha Musa

1 aKisha Musa akaupanda mlima Nebo kutoka tambarare za Moabu mpaka kilele cha Pisga, ng’ambo ya Yeriko. Huko Bwana akamwonyesha nchi yote: kutoka Gileadi mpaka Dani, 2 bNaftali yote, nchi ya Efraimu na Manase, nchi yote ya Yuda mpaka bahari ya magharibi,
Yaani Bahari ya Mediterania.
3 dNegebu na nchi yote kuanzia Bonde la Yeriko, Mji wa Mitende, hadi Soari. 4 eKisha Bwana akamwambia, “Hii ndiyo nchi niliyomwahidi Ibrahimu na Isaka na Yakobo kwa kiapo niliposema, ‘Nitawapa wazao wako.’ Nimekuruhusu uione kwa macho yako, lakini hutavuka kuingia.”

5 fNaye Musa mtumishi wa Bwana akafa huko Moabu, kama Bwana alivyokuwa amesema. 6 gMungu akamzika huko Moabu, katika bonde mkabala na Beth-Peori, lakini hakuna ajuaye kaburi lake lilipo mpaka leo. 7 hMusa alikuwa na umri wa miaka mia moja na ishirini alipofariki; hata hivyo nguvu ya macho yake haikufifia wala mwili wake haukudhoofika. 8 iWaisraeli wakaomboleza kwa ajili ya Musa kwenye tambarare za Moabu kwa siku thelathini, mpaka wakati wa kulia na kuomboleza ulipopita.

9 jBasi Yoshua mwana wa Nuni alijazwa roho ya hekima kwa sababu Musa alikuwa ameweka mikono yake juu yake. Kwa hiyo Waisraeli wakamsikiliza na wakafanya yale ambayo Bwana alikuwa amemwagiza Musa.

10 kTangu wakati huo, katika Israeli hajainuka nabii mwingine kama Musa, ambaye Bwana alimjua uso kwa uso, 11 laliyetenda ishara zote zile za miujiza na maajabu ambayo Bwana alimtuma kuyatenda huko Misri, yaani kwa Farao na maafisa wake wote na nchi yake yote. 12 mKwa kuwa hakuna mtu yeyote aliyewahi kuonyesha nguvu nyingi ama kutenda matendo ya kutisha ambayo Musa aliwahi kuyafanya mbele ya Israeli yote.
Copyright information for SwhKC